meneja mradi Focus Laurent akiangalia mahindi yaliyolimwa kwa kufata hatua moja na nyingi ambapo heka moja hutoa jumla maguni 25 mpaka 30 kwa kufata vipimo .
meneja mradi Focus Laurent akiwaonyesha wakulima wa Bulima kilimo bora kwa kulima kwa wakati na mvua za mwanzo.
Wahamasishaji wa kilimo cha kisasa,kupitia mradi wa Input Promotion
Programm(I.P.P) kanda ya magharibi kupitia kwa meneja mradi Focus Laurent akitoa maelenzo juu ya upandaji wa mbengu za mahindi katika kijiji cha chibiso wilayani kahama .
KAHAMA
Wakulima
katika halimashauri ya Ushetu wilayani Kahama wameaswa kuacha kilimo cha
mazoea ambacho hakina tija ukilinganisha na hali ya hewa inavyobadilika
badala yake watumie njia za kisasa ambazo zitaendana na mahitaji yao ya
maendeleo.
Wito
huo umetolewa na kaimu meneja bodi ya
Pamba kanda ya Magharibi Buluma Kalidushi alipokuwa akizungumza na wakulima wa
vijiji vya Chibiso na Mapamba katika siku ya wakulima shambani ambapo
aliwatembelea wakulima hao kwa lengo la kuhamasisha kilimo cha kisasa kwa
wakulima.
Kalidushi
amesema wakulima wanapaswa kufuata njia za kisasa kuanzia wakati wa kuandaa
mashamba,upandaji,utunzaji wa mazao na kuacha kutumia kilimo kilichozoeleka
kwani nyakati za sasa haziendani na awali kulingana na hali ya hewa si kwa
mazao ya chakula au biashara.
Kwa
upande wao wahamasishaji wa kilimo cha kisasa,kupitia mradi wa Input Promotion
Programm(I.P.P) kanda ya magharibi kupitia kwa meneja mradi Focus Laurent
amesema watashiriki na kuwaelimisha wakulima kufuata njia bora za kilimo cha
kisasa.
Nao
badhi ya wakulima wa vijiji vya Chibiso na Mapamba Charles Ng’imba na Pellagia
Simon ambao mradi huo wa I.P.P unaotekelezwa kwao wamewashukuru mafunzo
wanayopatiwa kwani kilimo cha njia bora za kisasa zinawaletea mavuno mengi
tofauti na awali.
Moja ya shamba la mfano katika kijiji cha Bulima kikundi cha songambele ni shamba la mfano la kikundi .
Baadhi ya wanakikundi cha songambele
wakiangalia zao la pamba ambalo limelimwa kwa hatu za kilimo cha pamba
katika kijiji cha bulima.
Wakinamama wa kikundi cha songambele wakiangali wadudu walibifu wa zao la pamba .
Afisa kilimo wa makampuni ya ipp
aliainama chini joseph mtalamu wa kampuni ya ipp ya umoja wa waunza
dawa za kilimo ,kungawa dawa wakiangalia mchi wa zaop la pamba .
kaimu meneja bodi ya
Pamba kanda ya Magharibi Buluma Kalidushi alipokuwa akizungumza na wakulima wa
vijiji vya Chibiso na Mapamba katika siku ya wakulima shambani alikuja mikono
moja ya shamba la mfano la zao la pamba
ambapo afisa kilimo toka makampuni ya ipp joseph akionyesha pamba
ilipandwa kwa kufata vipimo .
tunawapongeza sana kwa kazi iyo ambao munafanya uko kwa ajili yakulisha raia yote KAHAMA na watu zote ambao vithaa itakapofika
ReplyDelete