UFUGAJI - KAHAMA


 Ufugaji wa ng'ombe umekuwa ukifanywa tangu enzi za mababu zetu na haiwahi tokea mfugaji kujua kwa nini anafanya ufugaji. Sababu kubwa ni faida ziletwazo na ufugaji, ng'ombe kwa mfano amekuwa akimletea mfugaji faida zifuatazo:-
 1. Hutoa Nyama Nyama ya ng'ombe ni chanzo kizuri cha protini kwa binadamu na kila siku duniani kote huchinjwa nyama ya ng'ombe na huliwa na asilimia kubwa sana ya binadamu duniani. Mabucha mengi makubwa duniani ni kwa ajili ya uchinjaji wa ng'ombe na pengine ndo mabucha ya kwanza kuanzishwa. Hapa Tanzania machinjio yote makubwa ni kwa ajili ya ng'ombe. Hii inaonyesha namna gani nyama ya ng'ombe huhitajika na binadamu. Nyama ya ng'ombe ikiwa imening'inizwa

2. Humpatia mfugaji maziwa Mfugaji anafaidi moja kwa moja maziwa kwa kuyatumia pale nyumbani akiyanwa au akiyatumia kama sehemu ya chakula (mboga). Lakini pia maziwa yamesaidia sana kuinua kipato cha mfugaji hasa anayefuata kanuni za ufugaji kwa kuyauzaa.

Mbali na Shughuli za Kilimo, Wilaya ya Kahama Wananchi wake wamekuwa wakijishughulisha Mno na Ufugaji wa Kisasa wa Ng'ombe. kwa kuzingatia Mafunzo kadhaa ya ufugaji bora na Unenepeshaji wa Ngo'ombe na Pia ushauri kuhusu kuuza Ng'ombe hasa Waliochinjwa ili kupata faida ya Ngozi na wenyewe.

0 comments:

Post a Comment

Vita Kawawa

Vita Kawawa
Mkuu wa Wilaya ya Kahama

Popular Posts

About

Copyright © Kahama - Dc | Powered by Blogger
Design by Viva Themes | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com