Tumbaku - Chanzo Kikuu Cha Mapato Wilayani Kahama


Tumbaku  ni zao la kibishara linalolimwa na kuvunwa ili kutengeneza sigara,kwa mkoa shinyanga zao hili linalimwa kwa wingi wilayani kahama mkoa wa shinyanga.Ambalo pia nizao linaloongoza kwa mapato wilayani kahama ikifatiwa na madini(Dhahabu) yapatikanayo wilayani hapo.
 
Zao hili baada ya kuvunwa majani yake hukaushwa kwa kutumia majiko yenye kutumia kuni nyingi wakati wa kukausha tumbaku kabla ya kupaki na kuuza kwenye makampuni yanayonunua tumbaku kama ATTT, ALIANCE nk.
Mbali na Faida na Mapato Mengi yanayopatikana kutakana na Kilimo cha Zao Hili, kumekuwepo na Uhribifu mkubwa mno wa Mazingira unaosababishwa na ukatwaji wa miti hovyo kwa ajili ya kupata kuni. 
Baada ya kuvunwa kwa zao hilo la tumbaku wakulima wote hurudisha fikra zao katika msistu wa ushetu ubagwe ulioko wilaya ya ushetu( kahama)mkoa washinyanga ilikupata kuni kwa ajili ya kukaushia tumbaku na badala ya kuvuna kuni wao hutumia fursa hiyo kukata miti mikubwa kwaajili ya kukausha tumbaku pamoja na kuchana mbao kwa ajili ya biashara kinyume na sheri.
Jitihada za Makusudi zinafanyika na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo wakulima kuhusiana na Umuhimu wa kutunza Mazingira na njia Mbadala ya kupata Kuni kwa ajili ya Kukaushia Tumbuka na na miti ya Uvunaji Mbao.

0 comments:

Post a Comment

Vita Kawawa

Vita Kawawa
Mkuu wa Wilaya ya Kahama

Popular Posts

About

Copyright © Kahama - Dc | Powered by Blogger
Design by Viva Themes | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com